The Donge Grand Iftaar 2015

              "Tufuturu Na Yatima" 

 

 

By Mwana Wa Pate

 

Donge La Mombasa Welfare Group hosted a Grand Iftar this past Sunday in honor of the orphans that we’ve been visiting during this month of Ramadhan. It was a packed event that saw 150 orphans and 250 members of the Mombasa community sit together to break the  day’s fast together.
There was a live nasheed orchestra and Quran recitations presented by our little orphan angels. Speeches were also given by leaders of the local community including Hon. Abdulswamad, Suleiman Shahbal and Saad Faraj. Our very own treasurer,  Mbarak, MC’d the event with much enthusiasm and energy.
The volunteers worked very hard to see this event run seamlessly. Their efforts paid off- all our guests gave very positive feedback regarding the event. Unfortunately I couldn’t be there myself but we did have live streaming so I didn’t feel left out.
We had a busy Sunday and by midnight we (the organizers and volunteers) were very tired but very, very, happy.
If you donated or volunteered for this event, please accept my heartfelt gratitude for your  contribution.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

By Mbarak Salim Mbarak

 

Asslamu aleykum WanaKhairati wa Donge, nwanzo tumhidi Allah kwa wote mazuri na ya mafanikio Dongeni. Siku ya Jumapili tarehe 12.07.2015 kuanzia saa 4:30pm hadi 8:00pm huko ukumbini Diamond Jubilee Hall ilikuwa ni siku ya historia kuu, shamra shamra, furaha na raha, siku adhimu na adimu yenye kheri kemkem. Ni siku tulio ipatia jina maalum - 'Futurisha Yatima.'

 

Tulikuwa na Mwaliko Mkuu wa Iftaar ya Mayatima. Ni fahari, neema, thawabu na furaha isiyo kifana kwa kueka tena tabasamu katika nyuso za watoto na ndugu zetu mayatima! Sherehe hiyo ilihudhuriwa pia na Mgeni wetu wa Heshima Alhabeeb AbdulSwamad Shariff Nassir ambaye ni M'bunge wetu wa Mvita, pia Almahboob MCA wetu wa Bondeni/Tononoka Mheshimiwa Saad Faraj Ahmed alikuwapo, Mzee wetu wa Busara na Mfanya Biashara maarufu ambaye ni Mentor wetu Az-Zaeem Suleiman Shahbal alihudhuria na kufanikisha hafla na sherehe hii yetu ya Donge La Mombasa Welfare Group.

 

Markaz tatu za mayatima zilibahatika kupata mwaliko huu uliyoandaliwa hususan kwa ajili yao. Mayatima wa AlJazeera, VOK Bombolulu, Mayatima wa Suleiman, Mtopanga, na Mayatima wa Ummul Kheir, Jomvu Jitoni.

Kama kawaida ya hafla zetu, kulisomwa na mmoja wa mayatima wa AlJazeera Qur'an kuashiria mwanzo wa sherehe zetu, Qaswida na Anasheed zikafuata kutoka kwa mayatima na wasomaji maarufu Issa Sudi na Ahmed Masoud wa RadioSalaam na RadioRahma. Zawadi kemkem zilitolewa kwa mayatima wote karibu 130 mashaAllah. Tulikula, na wao wakala hadi tukatosheka. Nyuso zilijaa nuru za mayatima, walifurahi na huku wakitabasamu kila mmoja na kuridhika, hii ni ishara tosha kuwa swadaqa, amali na michango yetu yote ya hali na mali imetaqabaliwa - Yaa Rabb.

Huku tukiendelea na hafla, ndugu zetu walioko ngambo walikuwa wafuatilia kwa makini sherehe hizo kupia kwa mitandao moja kwa moja. RadioSalaam walipeperusha hewani hafla hii kuanzia mwanzo hadi tamati. Mwaandishi wa gazeti moja maarufu pia alikuwemo na kuchukuwa kumbukumbu zetu. Furaha yetu ilifika kilele pale Mwenyekiti wetu Mheshimiwa Kijana Cha Juma Bhalo pamoja na Mkewe Secretary wa Donge Mwana Pate walipotuletea ujumbe maalum na pongezi kutoka huko ng'ambo Uingereza, ujumbe ulichezeshwa kwa njia ya video kupitia kwa projector mbele ya halaiki iliyokuwemo. Naye MwanaIdara wetu Mpendwa Kareem Mohamed alikuwa nasi kiroho huko London na kutuwekea wazi yote yanayojiri hapo.

 

Ndugu na Meneja wetu mpendwa pia asiyechoka Laabied Mohammed Gurcharan alihakikisha kuwa maandalizi na wote waliohudhuria wako bardan wasalama. Kikundi chetu cha ualishi na maandalizi walifanya kazi ya ziada na kuona kuwa wageni wetu mayatima na alhaadhirina wako murtaahi kuanzia mwanzo hadi kuhitimisha, na kuhakikisha kuwa mayatima wote wa markaz tatu wamerudi kwao salama salmini.

Kwa bahati nzuri pia, tulisherehekea mazazi ya Mheshimiwa wetu AbdulSwamad pamoja na mayatima hao, keki mbili zenye logo ya Donge na sura ya Mheshimiwa zilikatwa. Vyakula vya kila aina alhamdulillah vilitandazwa. Sherehe hiyo ambayo mimi nilikuwa ndiye Master of Ceremony ilihitimishwa na dua kutoka kwa ndugu mpendwa Abdul Skandor kutoka Al-Imdaad Foundation Kenya ikiashiria kilele cha sherehe yetu ya 'FUTURISHA YATIMA.

​​Call us: +254706591911 or +447448855183

email: info@dongelamombasa.com

​Find us: Donge House, Near Masjid Ali - Kereketa, Behind Coast General Hospital

Mombasa Kenya

© 2013 by Donge La Mombasa Welfare Group

This site was designed with the
.com
website builder. Create your website today.
Start Now